Wakala waChuo
Cha Taifa Cha Utalii waendelea kukua
· Zamani ilijulikana kama Chuo cha Hoteli na Utalii
Forodhani
Na Beatrice Discoryce
Unapopita
katika Makutano ya Barabara ya Samorana Mtaa wa Shaban Robert, Jijini Dar es
Salaam, jirani na yalipo Makao Makuu ya Wizara ya Afya na Chuo Cha Usimamizi wa
Fedha (IFM), kuna jengo zuri jeupe, unaweza ukadhani kwamba hiyo ni hoteli ya
kifahari, la hasha, kumbe hapo ni Makao Makuu ya Wakala wa Chuo Cha Taifa cha Utalii
na Kampasi ya Bustani, sehemu ya wahitimu
wanataaluma ambao ni wachangiaji wa pato la Taifakwa wastani wa shilingi
trilioni mbili na ushee kwa mwaka.
Hapo ni
mahali pekee ambapo kijana wa Kitanzania anapohitimu masomo yake anatembea
kifua mbele pasi na shaka ya kupata ajira, kwani wahitimu wa chuo hicho ni lulu
serikalini na kwa wawekezaji katika sekta
ya Utalii.
Lakini
wengine hujiajiri na kuyanawirisha maisha yao, wengi wao hivi sasa wanamiliki
mighahawa, mahoteli na makampuni ya kitalii kona mbalimbali za nchi yetu.
Tanzania
kama nchi nyingine Duniani kote, kuna changamoto ya ajira kwa vijana, lakini ni
nadra sana kumpata kijana aliyehitimu katika taasisi hiyo akirandaranda mtaani
kutafuta ajira kwani kwani chuo kinazalisha vijana ambao wameiva kitaaluma,
ki-nadharia na ki- vitendo. Kizuri zaidi ni kuwa chuo hicho mali ya Umma,
heshima yake haijashuka tangu kianzishwe, miaka ya nyuma kilijulikana kama Chuo
cha Mafunzo ya Hoteli na Utalii
Forodhani na kilikuwa eneo la barabara
ya Kivukoni mahali ilipo Mahakama ya Rufaa.
Ili kuhakikisha
kwamba wahitimu wanakuwa bora, mafunzo ya vitendo huchukua asilimia 60 wakati
nadharia huchukua asilimia 40 iliyobaki, wakitengewa pia muda wa kutosha wa
kufanya mazoezi kazini.
Uongozi wa
chuo hicho unasema mwaka jana pekee takribani vijana 173 walihitimu katika Chuo
hicho, asilimia kubwa wameajiriwa wengine wamejiari na wengine wanaendelea na masomo ya juu vyuo mbalimbali.
“Tumewafuatilia
Wahitimu wetu na kubaini kuwa asilimia kubwa wamepata ajira katika sehemu
mbalimbali, wengine serikalini lakini wengi zaidi sekta binafsi ambako biashara
ya hoteli na Utalii kwa ujumla imepamba moto, vijana wetu wamebobea katika fani
za utunzaji na uaandaji wa vyumba,Mapishi,Uokaji,Uhudumiaji wageni,Uongozaji
watalii na Mapokezi ya wageni hotelini na Utalii,”
Kaimu Afisa
Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho Rosada Msoma, ambacho pia ni Wakala wa Serikali tangu
mwaka 2003 anafafanua kuwa wahitimu wetu wao wako kwenye sekta kiongozi katika
uchumi, sekta inayoshika nafasi ya tatu kwa kuliingizia Taifa pato kwa mwaka,
yaani sekta ya Utalii.
Wachumi
wanasema mapato katika sekta hiyo kwa mwaka 2013 yalikuwa ni Sh trilioni 2.96
baada ya kupokea watalii 1,095,884 yakiongezeka kutoka Sh. trilioni 2.69 za
mwaka 2012 zilizotokana na watalii 1,077,058 waliongia nchini.
“Kwa hiyo
ni jinsi gani unaweza kuona Chuo chetu kilivyo muhimu katika maendeleo ya sekta
hiyo hasa kwa kuzalisha vijana ambao wanaweza kazi zao kwa ufanisi mkubwa
kutokana na kusomeshwa vizuri ,”anasema.
Anabainisha
kuwa ubora wa mafunzo unatokana na ubora wa Waalimu ambao nao pia wamesomeshwa
vizuri na serikali.
“Tuna vifaa
vya kisasa kuliko chuo chochote cha aina ya kwetu hapa Afrika Mashariki, tuko
vizuri, ndiyo maana hata vijana wanapotoka hapa hawaangaiki kutafuta kazi,waajiri
wenyewe wanawakubali.
Anafafanua
kuwa Chuo chake kimesajiliwa na NACTE kutoa elimu kwa ngazi ya Stashahada na
Astashahada.
“Tunatoa
mafunzo bora kulingana na mahitaji ya soko,mafunzo ambayo pia yanamuwezesha
muhitimu si kuajiriwa tu na hata kujiajiri, wapo waliojiajiri na ambao kwa
kweli wanafanya vizuri sana kwenye biashara zao, na wengine ni wafanyabiashara
wakubwa katika sekta ya Utalii lakini wamepitia hapa hapa,” anasema.
Katika
kusaka elimu wapo wenye kiu ya kuendelea na mafunzo ya juu zaidi anasema baadhi
yao hivi sasa wako katika ngazi mbalimbali za viwango vya elimu kwa maana
wengine wanasomea Shahada ya kwanza.”
“Wako
waliopita hapa kwa sasa ni wasomi wazuri na wanafanya shughuli zao mbalimbali,
kwa kuwa hiki ni Chuo cha serikali, ni rahisi mhitimu kujiendeleza zaidi
kielimu,kwani ni chuo kinachotambulika,hivyo kuwa rahisi kwa wahitimu wetu kuendlea
na elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu.
Anasema
Chuo kina kampasi tatu ambazo zinatoa mafunzo katika ngazi ya Astashahadana Stashahada,
anazitaja kampasi hizo kuwa ni Bustani ambayo pia ni Makao Makuu ya Chuo hicho
ambayo inafundisha kozi Ukarimu (Hospitality) kampasi hii ina uwezo wa kuchukua
wanafunzi 360.
Kampasi
nyingine ni ya Temeke, yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 150, na inafundisha
kozi ya Utalii wakati ile ya Arusha inachukua wanafunzi 120 na inafundisha kozi
ya Ukarimu (Hospitality). “Jumla Wakala una uwezo wa kuchukua vijana wa mia
sita thelathini (630) hivi,” anasema.
Bi.Msoma
anafafanua kuwa kozi za Ukarimu ngazi ya Astashahada huchukua miaka miwili
ambayo hujumuisha masomo ya Mapishi (Food Production),Utoaji huduma ya vyakula
na Vinywaji, (Food and Beverage Services),Utunzaji Vyumba (Accomodation
Operations), Uokaji (Pastry and Bakery) na Mapokezi ya Wageni Hotelini ( Front
Office Operations).
Kwa ngazi
ya Stashahada anasema inajumuisha masomo ya Mapishi(Culinary Arts),Utoaji
huduma ya Vyakula na Vinywaji, Utunzaji na Ugawaji wa Vyumba (Rooms Division).
Kozi za Utalii
ngazi ya Astashahada anasema inajumuishamasomo
ya Uongozaji Watalii (Tour Guiding Operations) mwaka mmoja, Usafiri na Utalii
(Travel and Tourism) miaka miwili.Ngazi ya Stashahada inajumuisha Usafari naUtalii
(Travel and Tourisim) miaka miwili pia.
Bi.Msoma
anasema kuwa ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanamudu ushindani katika soko la
ajira ndani na nje ya nchi,chuo pia hufundisha masomo ya Kiingereza na
Kifaransa, TEHAMA (Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano), Ujasiriamali,Rasilimali watu na Huduma kwa mteja.
“Pia Wakala
hutoa kozi za muda mfupi kulingana na mahitaji ya wateja katika fani za Utalii
na Ukarimu,”
Anasema Chuo
pia hutoa huduma za Utafiti na Ushauri katika Nyanja za Utalii na Ukarimu.
Anabainisha
kwamba ili kutoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo, kampasi zote tatu,
Bustani,Temeke na Arusha hutoa huduma ya vyakula na kumbi za mikutano ambapo
huduma hizi huchangia pato la ndani la Wakala.
Anayataja
mafanikio ya Chuo hicho kuwa ni,kupanuka kwa Chuo, kwa maana ya kujitanua na
kuwa na majengo ya kutosha kufanyia shughuli zake za ufundishaji kwa nadharia
na vitendo.
Chuo kuwa
Wakala wa serikali mwaka 2003,Chuo kuwa na majengo mazuri na vifaa vya kisasa vyenye
technolojia ya hali ya juu katika kampasi kampasi ya Bustani.
Mengine ni
kupanuka kwa Chuo kutoka Kampasi moja yenye uwezo wa wanafunzi 150 kufikia
wanafunzi 630 kwa kampasi tatu, ambapo imeongeza uwezo wa kudahili kufikia wanafunzi
315 kwa mwaka.
Mengine ni
kuongezeka kwa programu za mafunzo ya usafiri na Utalii kwa ngazi ya cheti.
Kuanzishwa
kwa Programme ya Apprenticeship kwa kushirikiana na Sekta binafsi pamoja na
Shirika la Kazi Duniani (ILO). Programme inatoa
nafasi kwa kijana kufanya kazi na kusoma, pia anakuwa na uhakika wa
kupata ajiri mara anapofanikiwa kusoma.
Kuanzishwa
na kuimarishwa kwa ofisi ya Mrajisi na mitihani chuoni, ambapo kumepelekea
utoaji wa mafunzo katika viwango vya Baraza la elimu ya Ufundi(NACTE).
Programu za
mafunzo yatolewayo katika kampasi zote tatu zinatambuliwa na Baraza la Elimu ya
Ufundi (NACTE).
Ukarabati
wa hostel za kulala wanafunzi na kuongeza uwezo wake toka wanafunzi 60 hadi
wanafunzi 120.
Anasema
kwamba mwaka 2007 walikuwa na Kampasi moja tu iliyoko Temeke, baadaye
wakafungua kampasi Arusha na kisha mwaka 2011 wakafungua kampasi ya Bustani. “Ni
mafanikio makubwa sana kupanua huduma zetu,”
“Mafanikio
mengine ni ujenzi wa jengo letu la Makao Makuu chini ya ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Ufaransa(AFD),” Anasema kupatikana kwa Majengo ya Arusha kutoka
kwa wafadhili wa Hans Seidel Foundationpia
ni mafakio yalichochea ukuaji wa kasi wa Chuo chetu,”.
Kuhusu
historia ya Wakala, Wakala umerithi Chuo cha Mafunzo ya Hotel naUtalii (HTTI),
maarufu kama Chuo cha Hoteli na Utalii Forodhani, iliyoanzishwa mwaka 1969
chini kampuni ya hoteli ya Kiingereza ya Hallmark Hotels, lengo lake lilikuwa
ni kutoa mafunzo ya msingi kwa watumishi
mbalimbali wa Hoteli.
Taasisi
hiyo ilikabidhiwa mara ya kwanza serikalini mwaka 1977 kupitia Wizara ya
Maliasili naUtalii, kutokana na mahitaji ya kuboresha huduma na kukua kwa sekta
ya Utalii nchini.
Anasema Dira
ya Wakala ni kuwa kituo bora Afrika katika kutoa mafunzo bora katika fani za
Ukarimu na Utalii, na Dhima ya Wakala ni kutoa mafunzo bora utafiti na huduma
ya ushauri katika sekta ya Ukarimu na Utalii kwa kutumia watumishi wenye weledi
na vifaa vya kisasa ili kufikia matarajio ya wateja.
Wakala unatekeleza
majukumu yake kwakufuata Malengo ya Mpango Mkakati wa Wakala wa mwaka 2014/15
-2016/17 unaotekelezwa kwa sasa, Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999,Ilani ya
Uchaguzi ya Chama Tawala ya mwaka 2010-2015,Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa
2011-2016, na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025
Anasema Chuo ni Wakala
pekee wa Serikali unaotoa mafunzo katika fani za Ukarimu na Utalii. Hivyo
wanatoa wito kwa wazazi na walezi wa wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne,
kidato cha sita na wale wanaomaliza miaka mitatu VETA katika fani ya Ukarimu na
Utalii wachangamke fursa ya kujiunga na chuo chao.
Mwisho
No comments:
Post a Comment